Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha SShirika la Habari la Hawza, kikinukuu jarida la Mir’at al-Bahrain, serikali ya Bahrain haijaacha tena mwanya wowote wa kufikia makubaliano au kuishi pamoja na Mashia; imekata nyuzi za mwisho za mawasiliano nayo, na juhudi za kimedia zinazoshuhudiwa leo kwa lengo la kuthibitisha kinyume chake zimehukumiwa kushindwa tangu mwanzo. Msingi wa uhusiano kwa sasa umejengwa juu ya hofu, na mahusiano yaliyobaki yanafanya kazi kwa kiwango kile kinachofanana na “uhalali wa kula mzoga katika hali ya dharura.”
Serikali ya Bahrain haimlengi tena Mshia mmoja mmoja, wala mashambulizi yake hayajawekewa mipaka kwa watu maalumu. Mashtaka ambayo imeyatunga na mipaka myekundu ambayo imeivuka yamefanya kila Mshia, mahali popote alipo, wakati wowote na kutoka katika mwelekeo au madhehebu yoyote, kuonekana kama mtuhumiwa au mhalifu.
Wakati serikali inapolipa jukumu la kidini la khumsi na shughuli zinazohusiana na utoaji wa haki za kisheria za Kiislamu chapa ya “utakatishaji wa fedha”, kisha ikaliingiza katika orodha ya makosa ya jinai, hali ya kuwa faradhi hiyo ni miongoni mwa “matawi kumi ya dini” kwa Mashia wa Ja‘faria, kwa ufupi jambo hilo lina maana kwamba; kuabudu kwa mujibu wa madhehebu ya Kishia kumebadilishwa kuwa kitendo cha kijinai. Hivyo, raia Mshia kwa sasa amewekwa kati ya chaguo mbili: kuacha madhehebu yake au kukabiliwa na mashtaka ya jinai!
Ni ukosefu gani mkubwa zaidi wa haya kuliko kuyaweka mambo ya kisheria ya dini katika orodha ya makosa ya jinai, kana kwamba ni vitendo vya uhalifu visivyotofautiana na wizi, utapeli au makosa mengine yanayofanana na hayo? Kisha kwa ujasiri mkubwa, tuhuma hizo zielekezwe kwa wanazuoni watukufu ambao wamekuwa miongoni mwa watu wasafi zaidi na wenye heshima kubwa katika jamii, huku historia yao yenye kung'ara ikishuhudia uadilifu na usafi wao.
Hatua hizi zote zinakuja katika muktadha wa juhudi rasmi za kuidhalilisha Marjaiya na wanazuoni wa madhehebu ya Ja‘faria, pamoja na nia ya kuwavunjia heshima kwa kutoa maelekezo ya moja kwa moja ya kuchapisha picha zao kwa namna inayolenga kuwafanya waonekane wadogo na kudhoofisha hadhi yao mbele ya jamii.
Ama kauli rasmi zinazozungumzia uhamishaji wa fedha kwenda Iraq, Iran na Lebanon, na kuuhusisha na malengo ya kisiasa, si chochote isipokuwa ni jaribio jingine la kuhalalisha kuifanya ibada ya wazi ya kidini kuwa kosa la jinai kwa dhehebu zima; ibada ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa mamia ya miaka.
Baadhi ya wanazuoni waliokamatwa wanamiliki hati rasmi za uwakilishi kutoka kwa mafakihi maalumu katika nchi hizo, na kufikisha haki za kisheria kwa Mara'jii hao ni sehemu ya majukumu yao ya kidini. Inawezekana, kwa kurejea kwenye tovuti za Marjaiya ya juu mjini Najaf Ashraf, hususan ya Ayatullah Sayyid Ali Sistani kwa mfano, kufahamu maeneo yanayotumiwa fedha za khumsi na watu wanaostahiki kuzitumia, hilo ni bora kuliko kudai kwamba fedha hizo zinatumwa kwa vyama au mikondo ya kisiasa isiyopatana na serikali; madai ambayo kila mtu anajua sababu ya kuyasambaza katika mazingira ya sasa.
Maoni yako